Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amewateuwa watu mashuhuri kuimarisha msaada wa mataifa maskini duniani

Ban amewateuwa watu mashuhuri kuimarisha msaada wa mataifa maskini duniani

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameteuwa tume ya watu mashuhuri 10 kutoa ushauri juu ya msaada unaohitajika kusaidia mataifa maskini kabisa duniani kuweza kutekeleza malengo yao ya maendeleo kabla ya mkutano muhimu wa kimataifa juu ya matafifa yenye maendeleo madogo kabisa, LDC hapo mwakani.

Katika taarifa yake Bw Ban anasema wajumbe wa tume hiyo wamechaguliwa kulingana na hadhi yao ya kimataifa, ujuzi wao na dhamira yao ya dhati kwa maendeleo ya kimataifa.

Tume hiyo itakayoongozwa kwa pamoja na rais wa zamani wa Mali Alpha Oumar Konare na Jacques Delores rais wa zamani wa Kamisheni ya Ulaya itabuni hali ya kuwepo na dhamira ya kisiasa ili kusaidia mataifa 49 maskini kufikia malengo yao ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, teknolojia na kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.