Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unahitaji helikopta zaidi kuwasilisha msaada kwa waathiriwa wa mafuriko Pakistan

UM unahitaji helikopta zaidi kuwasilisha msaada kwa waathiriwa wa mafuriko Pakistan

Janga la mafuriko likiendelea huko Pakistan, idara za huduma za dhaura za Umoja wa Mataifa zinakadiria kwamba watu 800,000 wanaohitaji msaada kote nchini wanaweza kufikiwa kutumia njia za anga pekee yake.

Mpango wa Chakula Duniani WFP umesema unahitaji helikopta zaidi ili kuwaslisha msaada wa dhaura kwa wathiriwa wa mafuriko. Msemaji wa WFP Emilia Casella amesema, katika muda wa mwezi moja helikopta 5 zimeweza kuwasilisha msaada kwa watu 140 000, na hivyo mahitaji ni makubwa wanahitaji helikopta zaidi.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)

Katika tukio jingine idara ya wakimbizi ya Umoja a Mataifa inasema inabadilisha wito wake wa msaada kwa waathiriwa wa mafuriko ya Pakistan kufikia dola milioni 120 kutoka ombi la awali la dola milioni 40.

UNHCR inasema ombi hilo itaiwezesha kutoa hifadhi za dharura na msaada kwa watu milioni 2 katika kipindi cha miezi minne ijayo.