Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kukomesha ghasia za ngono kua silaha ya vita: UNICEF

Lazima kukomesha ghasia za ngono kua silaha ya vita: UNICEF

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, Anthony Lake, anasema shambulio la ubakaji wa zaidi ya wanawake na wasichana 150 huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linabidi kua onyo la kusitisha utumiaji wa ghasia za ngono kama silaha ya vita.

Katika taarifa yake, iliyotolewa Jumatano, Bw Lake anasema ukiukaji wa kikatili wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na ubakaji na ghasia za ngono zimekua janga kubwa huko DRC. Aliongeza kusema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba mashambulio mengi kama hayo yamefanyika bila ya kuripotiwa.

Mkuu wa UNICEF anasema athari zinazotokana na ghasia za ngono hazimaliziki kwa shambulio lenyewe, bali waathiriwa wengi huendelea kubaki na kidonda cha mwilini na akili kwa maisha yao yote.