Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtalaamu wa UM kwenda Msumbiji kukagua namna vyombo vya utoaji maamuzi vinavyotekeleza majukumu yake

Mtalaamu wa UM kwenda Msumbiji kukagua namna vyombo vya utoaji maamuzi vinavyotekeleza majukumu yake

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ambaye anahusika na masuala ya sheria na haki Bi Gabriela Knaul, anatazamiw kuzuru Msumbiji kwa shabaha ya kukagua namna vyombo vya utoaji haki na maamuzi nchini humo, vinavyotekeleza majukumu yake. Anatazamiwa kufanya ziara hiyo kuanzia Agosti 26 hadi September 4

Akiwa nchini humo, mtaalamu huyo ambaye hufanya kazi kwa uhuru atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo yale yanayohusika na utoaji wa haki na maamuizi ya kisheria, na kuangalia kwa kiwango gani wananchi wa kawaida wanaweza kuzifikia taasisi za maamuzi na zile za kisheria

Mtaalamu huyo ambaye anakwenda nchini humo kwa mwaliko wa serikali ya Msumbiji anatazamiwa kutoa mapendekezo na kuzishauri taasisi za maamuzi namna zinavyoweza kutenda kazi wa uhuru na haki.

Anatazamiwa pia kukutana na waandishi wa habari hapo September 4 Mjini Maputo ambapo atatumia fursa hiyo kuwasilisha mapendekezo yake.