Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhisho la haraka lahitajika kwa watu waliopoteza makwao nchini Bosnia

Suluhisho la haraka lahitajika kwa watu waliopoteza makwao nchini Bosnia

Mcheza filamu na balozi wa Umoja wa Mataifa Angelina Jolie ametoa wito kwa hatua kuchukuliwa kuwasaidia takriban watu 113,000 ambao hadi sasa hawana makwao miaka kumi na tano baada ya vita vya Bosnia.

Hadi sasa zaidi ya watu milioni moja wamerejea makwao nchini Bosnia huku shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR likichukua nafasi kubwa kurudi nyumbani kwa wakimbizi hao.