Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umelalamika vikali kutokana na ubakaji wa magengi unaofanywa na waasi mashariki ya DRC

UM umelalamika vikali kutokana na ubakaji wa magengi unaofanywa na waasi mashariki ya DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wake maalum wa kupambana na ghasia za ngono katika maeneo ya vita Margot Wallstrom, wamelaani vikali mashambulio ya ubakaji wa hivi karibuni na utumiaji nguvu dhidi ya zaidi ya watu 150 yaliyofanywa na waasi kwenye maeneo yenye ghasia ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wamesema mashamblio hayo yanaonesha kiwango utumiaji nguvu wa ngono ulivyoenea huko DRC na kuwa jambo la kawaida.

Bw Ban na Bi Wallstrom wamehimiza kwamba ni lazima kuwafikisha mahakamani wahusika na kuahidi watawasaidia wakuu wa DRC kupambana na hali ya kutohukumiwa wanaotenga ghasia kama hizo.

Katibu Mkuu alisema anampeleka mara moja naibu Katibu Mkuu Atul Khare kutoka idara ya shughuli za kulinda amani hadi eneo hilo ili kutathmini jinsi UM utajibu.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu inasisitiza juu ya haja ya makundi yote yenye silaha nchini humo kuweka silaha zao chini na kujiunga na utaratibu wa amani.

Karibu watu 154 walibakwa katika vijiji 13 kwenye wilaya ya Banamukira, Kivu ya Kaskazini kati ya Julai 30 na Ogusti 2.