Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wa kwanza kutoka Senegal wanawasili Darfur

Polisi wa kwanza kutoka Senegal wanawasili Darfur

Kikosi cha kwanza cha maafisa wa polisi kutoka Senegal waliwasili El-Fasher, kwa kipindi cha mwaka mmoja huko Darfur. Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kupeleka kikosi cha polisi kufanyakazi ya Umoja wa Mataifa.

Maafisa hao walipokelewa na kamishna mpya wa polisi wa UNAMID James Oppong Boanuh, na watapelekwa kufanyakazi huko El Genina, Magharibi ya Darfur.

Senegal inakua nchi ya nane kuchangia kikosi cha polisi cha UNAMID, cha maafisa 1819. Mataifa mengine ni Bangladesh, Misri, Jordan, Indonesia, Nepal, Nigeria na Pakistan.