Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inawasaidia waathiriwa wa kimbunga Agatha huko Guatemala

IOM inawasaidia waathiriwa wa kimbunga Agatha huko Guatemala

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM pamoja na washirika wake huko Guatemala limeweza kutoa mikoba ya dharura 900 kwa waathiriwa wa kimbunga Agatha.

Msemaji wa IOM Jared Bloc akizungumza na waandishi habari mjini Geneva anasema IOM na washirika wake wa Umoja wa MataIfa wametoa misaada isiyo ya chakula kwa waathiriwa.

(SAUTI YA BLOCH)

Amesema, msaada ambao si wa chakula ni pamoja na kukarabati majengo kumi ya serikali yanayotumiwa kama hifadhi za dharura.