Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inawapatia watu milioni 1.5 maji kila siku Pakistan

UNICEF inawapatia watu milioni 1.5 maji kila siku Pakistan

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linaendelea na huduma zake za dharura kwa kutoa maji, chakula huduma za afya na kuwalinda watoto huko Pakistan.

Kwa upande wa maji masafi inatoa lita milioni 1.5 kwa watu milioni 1.5 kila siku hasa katika maeneo ya kaskazini. Msemaji wa UNICEF Marco Rodriguez anasema:

(SAUTI YA MARCO RODRIQUEZ)

Wakati huo huo UNHCR inasema maji ya mafuriko yamekua yakienea katika maeneo mapya huko Kusini mwa Pakistan mnamo siku chache zilizopita na kupelekea watu kukusanyika katika maeneo mbali mabli ya Jimbo la Sindh.