Maelfu ya wakazi wakimbia makazi wakati mafuriko makubwa yanazidi kuenea Pakistan ya kusini - UM

24 Agosti 2010

Idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne kwamba hali katika jimbo la kusini mwa Pakistan la Sindh inaendelea kuzorota kutokana na wimbi la pili la mafuriko yanayozomba vijiji na kuharibu mashamba.

OCHA inasema kiasi cha hekta milioni 3.2 za mashamba ya kilimo zimeharibika hadi hivi sasa kote nchini humo na mifugo laki mbili kuzama.

Kwa upande mwngine idara ya Chakula ya Umoja wa Mataifa WFP inasema, idadi ya watu ambao imeweza kuwasiadia hadi sasa imefikia milioni 1.75 na inalenga kuwahudumia watu 150,000 kwa siku hali ikiruhusu. WFP ina helikopta tatu zinazodondosha biskuti zenye lishe, na inatarajia kufanya safari 30 za helikopta kwa wiki.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter