Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP huenda ikapunguza msaada wa chakula Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na upungufu wa fedha

WFP huenda ikapunguza msaada wa chakula Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na upungufu wa fedha

Maelfu na maelfu ya watu wanakabiliwa na hatari ya utapiamloo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa idara ya Chakula ya Umoja wa Mataifa WFP haitoweza kupata fedha zinazohitaika kuendelea na mpango wa kugawa chakula.

WFP inaupungufu wa dola milioni 15 katika kipindi cha miezi minane ijayo kuweza kutoa msaada wa chakula kwa watu laki sita wasio na chakula na kukabiliwa na utapiamloo katika maeneo yaliyoathiriwa na vita huko kaskazini mwa nchi.

Msemamai wa WFP huko Geneva Emilia Casella, anasema ikiwa hawatopata fedha katika muda wa miezi miwili ijayo watalazimika kupunguza msaada kwa wakimbizi laki moja pamoja na walopoteza makazi yao na hata kusitisha mpango kamili wa chakula kwa watu wengine.

"Kwa wakati huu utapiamloo sugu ni kiasi ya asili mia 37.5, utapiamloo ulokithiri ni asli mia 10.2 hii ni nchi inayohitaji sana msaada ingawa mdogo lakini ni muhimu. Hivyo WFP inawaeleza wafadhili na watu juu ya jinsi hali ilivyo mbaya, na huwenda tukalazimika kusitisha msaada kwa watu maskini kabisa".

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa 2009, wakati wakimbizi karibu elfu 17 wa Congo walipokimbilia wilaya ya Lobaye huko kusini mwa nchi. WFP inatoa pia msaada kwa wakimbizi wengine elfu 9 wa Sudan na elfu 14 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.