Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi maalum wa KM Somalia amelaani vikali shambulio la kujitoa mhanga Mogadishu

Mwakilishi maalum wa KM Somalia amelaani vikali shambulio la kujitoa mhanga Mogadishu

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia, Balozi Augustine Mahiga amelaani vikali kabisa shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya hoteli moja mjini Mogadishu Jumanne asubuhi ambapo raia kadhaa pamoja na wabunge wanne waliuwawa.

Balozi Mahiga alisema vitendo hivi viyovu na vya kikatili vyenye kulenga kusababisha umwagikaji damu mkubwa wa watu wasio na hatia havifahamiki hata kidogo.

Alisema walohusika na mauwaji haya wana nia ya kusababisha uharibifu na uchungu kwa watu wa Somalia. Alisema hata hivyo hawatafanikiwa na kampeni yao ya utumiaji nguvu. Mwakilishi maalum Mahiga alitoa rambi rambi zake kwa famlia za waathiriwa na serikali ya Somalia.