Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa misaada ya kiutu wa UM asema hali inazidi kuwa mbaya Darfur

Mkuu wa misaada ya kiutu wa UM asema hali inazidi kuwa mbaya Darfur

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na shughuli za kibinadamu ameyahimiza makundi yanayohasimiana katika eneo la Darfur nchini Sudan kuepusha vitendo vya uhasama na vitisho dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kiutu ili wafanyakazi hao waweze kuendelea na utoaji wa huduma na kuwafikia wathirika wa mapigano

Akitoa taarifa ya maendeleo ya misaada ya kiutu mbele ya kikao cha Baraza la Usalama, mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu John Holmes amesema kuwa hali ya upekekaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Darfur imeanza kuzorota tena kutokana na kuripuka upya kwa machafuko baina ya wapiganai wa serikali na vikundi vya waasi

Ameeleza kuwa makambi yaliyotumika kuwahifadhi ikiwemo ile ya Kalma camp imeathiriwa vibaya kutokana na mapigano hayo, na mamia ya watu waliokuwa wakiishi hapo wamelazimika kukimbia upya.