Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa kujitegemea wa UM kwenda Vietnam kufanya tathmini ya hali ya umaskini wa kupindukia

Mjumbe wa kujitegemea wa UM kwenda Vietnam kufanya tathmini ya hali ya umaskini wa kupindukia

Mjumbe wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu na umaskini wa kupindukia anatazamiwa kuzuru Vietnam ili kufanya tathmin ya hali mbaya ya umaskini unavyowaandama wananchi wa eneo hilo huku pia akiangazia namna serikali inavyokabiliana na tatizo la umaskini.

Mjumbe huyo Magdalena Sepúlveda ambaye anatazamia kukusanya taarifa za awali kuhusiana na umaskini unavyowaathiri wananchi wa kawaida, atafanya ziara hiyo kuanzia August 23 hadi 30.

Mjumbe huyo ambaye amekuwa akijihusisha na masuala ya umaskini na haki za binadamu tangu mwaka 2008,amesema hiyo itakuwa ni fursa muhimu kupitia mipango inayoofanywa na serikali ili kuwakwamua wananchi wake na wakati huo huo inatoa mwangaza sahihi wa serikali kutathminiwa namna alivyoweza kupiga hatua kwenye utekelezaji wa mipango yake.