Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa utafiti wa meli za msaada kwa Gaza umewasili Uturuki

Ujumbe wa utafiti wa meli za msaada kwa Gaza umewasili Uturuki

Tume ya uchunguzi ya wajumbe watatu waloteuliwa na rais wa Baraza la Haki za binadam kuchunguza tukiyo la mashambulizi dhidi ya meli za misaada huko Gaza imeanza kazi zake siku ya Jumapili.

Ujumbe huo umeanza ziara ya wiki mbIli nchini Uturuki, baada ya wiki mbili za mikutano na matayarisho mjini Geneva. Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva anasema watalamu wa kisheria ni kiufundi wanafuatana na ujumbe huo ambao unatarajia kuchuguza meli ya Mavi Marmara ambapo abiria wanane kutoka Uturuki waliuwawa hapo Mei 31 mwaka huu.

Ujumbe huo wa waatalamu wa vyeo vya juu ulianza kuwahoji mashahidi mjini London na Geneva wiki iliyopita kwa lengo la kukusanya habari halisi kuweza kutathmini ukweli wa mambo wa tukio hilo.