Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO inadhimisha siku ya kimkataifa ya makuimbusho ya bishara ya utumwa

UNESCO inadhimisha siku ya kimkataifa ya makuimbusho ya bishara ya utumwa

Ulimwengu umeadhimisha siku ya kimataifa ya kukumbuka biashara ya utumwa siku ya Jumatatu kwa sherehe zilizoongozwa na Idara ya elimu na sayansi ya Umoja wa mataifa UNESCO.

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Bi Irina Bokova alisema katika mwaka huu wa kimatiafa wa kuleta pamoja utamaduni mbali mbali, makumbusho ya biashara ya Ottumwa ni moja wapo ya maafa mabaya katika historia ya ubinadamu inatulazimisha kutafakari juu ya njia za kupunguza na kuondoa kabisa makumbusho machungu kama haya.

Tangu kuanzishwa kwa siku ya Kimataifa ya ukumbusho wa bishara ya utumwa 1998, UNESCO imeweza kuchangia katika mpango wa kutafakari na kutafuta njia na uwezo wa kuwepo na maridhiano na upatanishi wa watu kupitia maafa ya kihistoria yanayowahusu wote.

Bi Bokova alitoa wito kwa wadau wote wa UNESCO, pamoja na wakuu wa mataifa, mashirika ya kimataifa na yasiyo ya Kiserikali kutoa nafasi ya mabadiloshano ya mawazo juu ya uhumumu na faida za mchanganyiko wa utamaduni.