Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kaskazini mwa Cameroon imeongezeka

Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kaskazini mwa Cameroon imeongezeka

Idara ya afya duniani WHO inaripoti kwamba kuna watu 2,849 waloambukizwa na kipindupindu huko Cameroon kukiwepo na watu 222 walofariki tangu mwezi wa Mei.

Inaripotiwa kwamba ugonjwa huo umeenea katika majimbo ya kaskazini ya Nigeria na nchi jirani ya Niger.

Mratibu wa WHO kwa ajili ya kipindupindu huko cameroon Dr Claire-Lise Chaignat anasema kiwango cha vifo kutokana na kipindupindu katika nchi hizo ni ya juu sana kulingana na kiwango cha wastan cha asili mia 1.0

Maafisa wa Cameroon wanalaumu pombe ya kienyeji kwa kuenea kwa uganjwa huo, lakini Dk Chaignat anasema kipindupindu ni ishara ya ukosefu wa maji masafi ya kunywa.