Umoja wa Mataifa wataka kuwepo kwa utulivu baada ya kutangazwa majina ya wagombea wa urais nchini Haiti

23 Agosti 2010

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Haiti vimetoa wito kwa wananchi kuheshimu sheria za uchaguzi baada ya kutangazwa kwa majina ya wagombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kundaliwa mwezi Novemba mwaka huu.

Tume ya uchaguzi nchini Haiti hapo jana ilichapisha majina ya wagombea 19 ambao inasema watagombea kiti cha urais mnamo tarehe 28 mwezi Novemba na kuondoa majina ya wagombea wengine 15 ambao inasema hawajahitimu kugombea kiti hicho akiwemo mwanamuziki maarufu wa mziki wa hip hop Wyclef Jean. Kupitia ujumbe uliotolewa kwenye mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince na vikosi vya kulinda Amani nchini humo MINUSTAH, ni kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki. Vikosi hivyo vimewataka wagombea wa kiti hicho kuweka maanani Maisha ya raia wa Haiti wasio na makao na kuweka kando masuala ya kibinafsi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter