Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washukiwa wawili wa mauaji ya wanajeshi wa MONUSCO wakamatwa DRC

Washukiwa wawili wa mauaji ya wanajeshi wa MONUSCO wakamatwa DRC

Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limewatia nguvuni watu wawili wanaoshukiwa kuwauwa wanajeshi wa India wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO.

Watu hao wamekamatwa jana Alhamisi baada ya kundi la watu wenye silaha kuvamia kituo cha MONUSCO kwenye eneo la Kirumba jimbo la Kivu ya Kaskazini na kuwauwa kwa visu wanajeshi watatu na kujeruhi wengine saba.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Congo meja Vianney Kazarama mmoja wa washikiwa hao amekiri kuhusika na mashambulizi dhidi ya MONUSCO.Takriban wanajeshi 4000 wa India ni sehemu ya mpango wa MONUSCO nchini Congo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alilaani vikali mauaji hayo na kuitaka serikali ya Congo kuanzisha uchunguzi wa haraka na kuwatia hatiani wahusika.