Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imeonya juu ya athari za mafuriko kwa mifugo Pakistan

FAO imeonya juu ya athari za mafuriko kwa mifugo Pakistan

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kwamba mbali athari kubwa zilizosababishwa na mafuriko ya Pakistan kwa binadamu, mifugo wengi wamekufa au wako katika hatari na msaada wa haraka kwa ajili ya kuwalisha wanyama unahitajika.

FAO inasema kwa kuwanusuru wanyama hao pia itasaidia kupunguza athari kubwa zaidi za kiuchumi. Shirika hilo linasema hadi sasa takribani mifugo laki mbili ikiwemo ng'ombe, kondoo, nyati, mbuzi na punda imethibitishwa kufa au kutojulikana ilipo, lakini idadi kamili inaweza kuwa kubwa zaidi labda mamilioni.

FAO inasema katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika sana na mafuriko mifugo kama kuku yote imekufa na mamilioni ya mifugo iliyonusurika inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula na hivyo kuiweka kwenye hatihati sekta nzima ya mifugo ya Pakistan.