Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kufufua vituo vya afya Pakistan:WHO

Ni muhimu kufufua vituo vya afya Pakistan:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema athari za kiafya kutokana na mafuriko nchinin Pakistan ni kubwa sana.

Shirika hilo linasema hii ni kutokana na kusambaratishwa kabisa kwa vituo vingi vya umma vya afya na hivyo kuongeza hatari ya waathirika wa mafuriko hayo kupata magonjwa. Dr Daniel Eduardo Lopez Acuna ni mkurugenzi wa mipango, sera na udhibiti wa misaada wa WHO.

(SAUTI YA DR EDUARDO WHO)

Ameongeza kuwa hofu kubwa ya WHO hivi sasa ni hatari ya kuzuka magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya maji ya kunywa kutokuwa safi na salama, uchafu mwingi wa mazingira na watu wenyewe, ukosefu wa chakula, malazi, mrundikano wa watu, kutokuwepo na fursa ya kupata huduma muhimu za afya na kuchelewa kubaini mapema mlipuko wa magonjwa.