Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Laurean Rugambwa kuhusu umuhimu wa wahisani

Mahojiano na Laurean Rugambwa kuhusu umuhimu wa wahisani

Nini umuhimu wa siku ya wahisani na wahisani wenyewe? katika kuadhimisha siku hii ya kiamatifa ya wahisani ? Zipi shughuli na changamoto wanazokabiliana nazo?

Mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha amezungumza na Laurean Rugambwa ambaye ni mratibu wa shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu ICRC katika kanda ya Afrika.

Rugambwa anasema wahisani wanakabiliwa na changamoto kubwa hususani wanapohudumu kwenye maeneo ya vita na migogoro, lakini kwanza anaeleza umuhimu wa siku hii ya wahisani kimataifa na kwa shirika lao, uangana nao.