Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zipi changamoto zinazowakabili wahisani duniani?

Zipi changamoto zinazowakabili wahisani duniani?

Wakati dunia leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi wa hisani au wato misaada, bado kuna changamoto nyingi kutekeleza majukumu yao.

Mashirika mengi ya hisani, watu binafsi na makundi mbalimbali wamekuwa wakikabiliwa na adha katika utendaji kazi wao, kama ukosefu wa fedha, vitendea kazi, matatizo ya usalama kama kutekwa na hata kuuawa.

Mwandishi wetu wa Nairobi Kenya na pembe ya Afrika Jason Nyakundi ametuandalia taarifa hii kuhusu siku ya wahisani.