Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umewataka vijana kuwa msitari wa mbele kuleta maelewano

UM umewataka vijana kuwa msitari wa mbele kuleta maelewano

Mkutano wa pili wa Kimataifa uliowahusisha vijana wenye ushawishi kwenye jamii zao umemalizika katika Mji Mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur, kwa kutolewa mwito kwa vijana hao kuongeza sauti zao ili kukaribisha hali ya maelewano.

Mkutano huo uliwajumuisha maelfu ya wanafunzi kutoka nchi 60, umehimiza namna jamii inavyopaswa kujongeleana na kuongeza maelewano kwa shabaya ya kuzika hitilafu za kijamii. Wakati akifunga mkutano huo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika masuala ya habari na mawasiliano Kiyo Akasaka alipongeza umashuhuri wa wanafunzi hao kushiriki kwenye mijadala iliyoangazia masuala ya mafungamano ya dini pamoja na  jamii yenye kufuata siasa zenye itikadi kali.

Wanafunzi hao walizingatia pia juu ya kukabiliana na migogoro inayoendelea kujitokeza mara kwa mara katika maeneo mbalimbali. Mwishoni mwa mkutano wao, wanafunzi hao walichukua jukumu la kujizoesha na masula ya mahusiano ya kimataifa na diplomasia.