Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

St Lucia yawa nchi ya 113 kujiunga na mahakama ya ICC

St Lucia yawa nchi ya 113 kujiunga na mahakama ya ICC

Saint Lucia imeongerza idadi ya nchi ambazo zimeridhia mkatana wa kuanzishwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

ICC ilianzishwa ili kuwahukumu watu wanaoshutumiwa kwa makosa makubwa kama mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Nchi hiyo ya Caribbean imetia sahihi mkataba wa Roma wa 1998 na kuwa mwanachama wa 113 wa mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague Uholanzi.

Mahakama hiyo hivi sasa inafanya uchunguzi katika mataifa matano ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jimbo la Darfur Sudan, Kaskazini mwa Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Kenya.