Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo vya Israel ni adha kubwa Gaza:WFP na OCHA

Vikwazo vya Israel ni adha kubwa Gaza:WFP na OCHA

Ripoti ya pamoja ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema vikwazo vya ardhini na baharini vya Israel dhidi ya ukanda wa Gaza vina athari kubwa za kibinadamu.

Ripoti hiyo inasema vikwazo hivyo vya Israel vilivyowekwa tangu mwaka 2007 vimeleta athari kubwa kwa usalama na maisha ya watu takribani 180,000, ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa utu wa mtu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo katika miaka kumi iliyopita jeshi la Israel limeongeza vikwazo kwa adhi ya kilimo Gaza na shughuli za uvuvi katika mwambao wa ukanda wa Gaza. Israel inasema imeweka vikwazo hivyo kwa ajili usalama na hasa kuzuia mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha ya Wapalestina.