Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kutathmini athari na msaada wa mafuriko Pakistan

UM kutathmini athari na msaada wa mafuriko Pakistan

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa alasiri ya leo linatathimini athari zilizosababishwa na mafuriko nchini Pakistan na msaada unaohitajika kwa mamilioni ya waathirika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozuru Pakistan mwishoni mwa wiki iliyopita aliahidi kuchagiza misaada ya haraka watu takriban milioni 20 ambao wengi wamepoteza jamaa zao, nyumba zao na mali zao.

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kuongeza misaada yake Daniel Toole mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kanda ya Kusini mwa Asia anasema shirika lake litaongeza mara tatu msaada wake .

Ameongeza kuwa ombi la msaada la awali lilikuwa ni kwa watu zaidi ya milioni tatu na sasa idadi ya watu imeongezeka na kuwa zaidi ya milioni 20.

(SAUTI YA DANIEL TOOLE)