Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kusaidia masuala ya hisani kwa kujali mazingira

UM kusaidia masuala ya hisani kwa kujali mazingira

Katika kuzingatia masuala ya wahisani shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP limeanzisha kituo cha taarifa kwenye wavuti kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira wakati wa shughuli za misaada ya kibinadamu.

Uharibifu huo ni ule unaotokana na majanga ya asili, vita na migogoro mingine. Kituo hicho kitajukuisha kanuni, nyaraka za mafunzo, taarifa za matukio yaliyotokea na nyezo zingine na kina lengo la kutumika kama muongozo kwa wafanyakazi wa hisani. UNEP inasema licha ya jukumu kubwa la wahisani wakati wa migogoro, mambo kama ya kukata miti kwa ajili ya kutoa malazi na kuni za kupigia na takataka vinaweza kuwa kikwazo kwa mafanikio ya shughuli za misaada ya kibinadamu.

UNEP inasema mfano mzuri ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako ukumbwa wa makazi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa nchi hiyo umesababisha athari kwa viumbe vya porini kama kwenye mbuga ya Virunga, ukataji miti na pia uharibifu wa rasilimali zingine.