Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya wahisani, wanajitolea kwa ajili ya wengine

Leo ni siku ya kimataifa ya wahisani, wanajitolea kwa ajili ya wengine

Leo ni siku ya kimataifa ya wahisani ambao hujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wengine.

Wakati ikiadhimishwa siku hii pia Umoja wa Mataifa unaadhimisha mwaka wa saba tangu shambulio la bomu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Baghadad Iraq. Siku hii imetengwa maalumu kwa ajili ya waliopoteza maisha yao katika kujitolea.

Pia ni katika kutoa msisitizo wa hali ya kibinadamu na changamoto zake kote duniani ikiwa ni pamoja na vitisho dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo ya vita, changamoto za kuwafikia wanaohitaji msaada na ongezeko la ugumu wa mazingira ya kibinadamu. Lakini je wafanyakazi wa hisani wenyewe wansemaje? Mtanzania huyu anahudumu nchini Liberia

(SAUTI MTANZANIA LIBERIA )

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wafanyakazi wa hisani wanasaidia watu ambao wamepitia matatizo mengi ili kurejea katika maisha yao ya kawaida.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Siku ya wahisani mwaka huu ina malengo makuu matatu. Kwanza ni kuutanabaisha ulimwengu kuhusu mahitaji ya kibinadamu kote duniani, kasha kuelezea kwa lugha rahisi na mtazamo mwepesi kazi ya uhisani inajumuisha nini na mwisho ni kuwakumbuka waliopoteza maisha yao katika kazi za hisani. John Holmes ni mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu ansema dunia inakabiliwa na changamoto kubwa katika siku zijazo kwa masuala ya kibinadamu.

(SAUTI  HOLMES)

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza Agosti 19 kuwa siku ya kimataifa ya wahisani , miaka miwili iliyopita ili kukumbnuka shambulio la bomu la Canal Hotel mjini Baghad Iraq ambapo wafanyakazi 22 wa Umoja wa Mataifa waliuawa na wengine zaidi ya 150 walijeruhiwa.