Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Palestina na Israel huenda wakaanza tena mjadiliano:UM

Palestina na Israel huenda wakaanza tena mjadiliano:UM

Kuna ishara kwamba huenda Palestina na Israel zikaafikiana kushiriki kwenye mazungumzo ya moja kwa moja kwa ajili ya kutanzua mzozo wa mashariki ya kati kufuatia juhudi zinazoendelea kufanywa sasa.

Naibu Mkuu wa Kitendo cha masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa Oscar Fernandez-Taranco amelimbia Baraza la usalama kwamba pande zote mbili kwa sasa zingali zikijadiliana katika vikao vya ndani kuamua kama zinaweza kupiga hatua na kuwa na majadiliano ya moja kwa moja.

Amesema Umoja wa Mataifa unakaribisha hali hiyo na kuzihimiza pande hizo kuongeza juhudi na kuzingatia utashi uliopo sasa anokusudia kutia dira kamili ya utanzuaji wa mzozo huo wa mashariki ya Kati. Mazunguzmo hayo yanasimamiwa na pande nne, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani.