UM kutumia michuano ya Olimpiki kuwaasa vijana kuhusu ukimwi
Umoja wa Mataifa umetangaza mpango maalumu unakusudia kuongeza msukumo wa uelewa kwa vijana dhidi ya maambukizi ya Virusi vya HIV ambao wanabeba asilimia 40 ya maambukizi hayo, pamoja na kupiga vita vitendo vya unyanyapaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibé amesema kuwa Umoja wa Mataifa Utaanza kushirikiana na kamati inayoandaa michuano ya Olympic ya vijana inayoanza mwishoni mwa juma huko Singapore kwa kuzingatia kuwa michuano hiyo itawakusanya vijana wenye ushawishi na msukumo wa kuweza kubadilisha hulka za vijana wenzio.
Chini ya mpango huo umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika ya kiraia utatoa mafunzo njia ya semina kwa vijana hao. Maeneo yatakayotiliwa mkazo ni pamoja elimu ya makuzi kwa kijana, afya ya uzazi na maeneo yanayohusika na vitendo vya unyanyapaa.
Umoja huo wa Mataifa umesisitiza kuwa lazima kuanza sasa kuwatia msumo vijana ili washiriki kwenye mapinduzi ya kweli ya kuzuia maambukizi kama ulimwengu unataka kufikia shabaya ya kutokuwa na maambukizi mapya.