Skip to main content

Popo wako hatarini Urusi baada ya moto wa msituni

Popo wako hatarini Urusi baada ya moto wa msituni

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP leo limeonya kwamba maisha ya aina 30 za popo nchini Urusi yako hatarini kufuatia moto wa msituni wa hivi karibuni.

UNEP inasema moto huo ambao ulilikumba eneo kubwa la Urusi umeharibu makazi ya popo hao na wengi maisha yao yatakuwa hatarini. Picha za satellite za hivi karibuni zimeonyesha kuwa ekari zaidi ya milioni moja zimeharibiwa vibaya na Magharibi mwa Urusi ambako ni moja ya maskani muhimu kwa mazalia ya aina 30 za popo nchini humo.

Kwa mujibu wa serikali ya Urusi moto huo ambao umekatili maisha ya watu 50 , umeteketeza pia ekari 40,000 za hifadhi ya misitu. UNEP inasema moto huo una athari kubwa kwa idadi ya popo wanaohama ambao ambao sasa watakabiliwa na matatizo ya makazi.