Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya afya Afghanistan inahitaji kuwezeshwa:WHO

Sekta ya afya Afghanistan inahitaji kuwezeshwa:WHO

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahisani mwakilishi maalumu wa shirika la Afya duniani WHO nchini Afghanistan Peter Graaff amesema sekta ya afya nchini Afghanistan imeomba kuimarisha uwezo wa kuwafikia maelfu ya raia wan chi hiyo wanaohitaji msaada wa huduma ya afya.

Ameongeza kuwa sisi jumuiya ya afya tunawasaidia watu tunaoweza kuwafikia, hii ikimaanisha kwamba kama hatuwezi kuwafikia basi hatuwezi kuwasaidia. Amesema licha ya changamoto za kiusalama wahudumu wa afya wamekula kiapo cha kuyaweka maisha yao hatarini ili kutoa huduma ya afya kwa kila mwanaume, mwanamke na mtoto nchini Afghanistan.

Amesema fursa ya kuwafikia walengwa na huduma szenyewe ni muhimu sana katika nchi hiyo iliyoghubikwa na migogoro ili kunusuru maisha ya watu. Afghanista imewaomba wanaodhibiti na kuhusika na kuwawezesha kupata fursa hiyo kwa kuheshimu kanuni za kimataifa . Afghanistan ni moja ya nchi zenye mtatizo makubwa ya kibinadamu duniani ambapo watotowa chini ya miaka mitano na kina mama wako kwenye hatari kubwa ya kufa kuliko kwingineko duniani.