Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuakabiliana na ukimwi kwa wahamiaji Afrika

IOM kuakabiliana na ukimwi kwa wahamiaji Afrika

Shirika linalohusika na uhamiaji la kimataifa IOM kanda ya kusini mwa africa kwa ushirikiano na shirika la kimataifa kuhusu mandeleo nchi Sweden (sida) pamoja na wizara ya mambo ya kigeni nchini Norway yametangaza upanuzi wa ushirikinao katika harakati za kukabiliana na virusi vinavyosababisha maradhi ya ukimwi hadi africa masharuiki.

Mpango huo ambao kwa sasa unajulikana kwa jina PHAMESA utazisaidia nchi za mashariki na kusini wa afrika kukabiliana na hatari zinazotokana na uhamiaji yakiwemo maradhi ya ukimwi. mpango huo utawalenga wahamiaji wanaofanya kazi, wale waliolazimishwa kuhama pamoja na wahamiaji wasi na wakati.

Mpango huo wa PHAMESA utawaleta pamoja washika dau kusini mwa na mashariki mwa afrika zikiwemo nchi za Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo, Angola, Kenya, Lesotho, Mauritius, Musumbiji, Namibia,Tanzania, Afrika kusini, Swaziland, Uganda na Zambia.