Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Baraza la usalama amaliza ziara Congo Brazzaville

Rais wa Baraza la usalama amaliza ziara Congo Brazzaville

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amekamilisga ziara rasmi ya siku tatu nchini Congo iliyojumuisha pia sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa taifa hilo.

Ali Treki pia alihudhuria waride la kijeshi na la raia lililoandaliwa katika mji mkuu Brazzaville na kuwa mgeni mkuu mwaalikwa wa rais wa kongo Dennis Sassou Nguesso. Baada ya kuwasili nchini kongo tarehe 13 mwezi huu Treki alijadiliana masuala kadha na rais sassou nguesso na kukutana pia na wakuu wa idara mbali mbali za serikali na watu wengine mashuhuri.

Wakati huo rais Nguesso alikubali mwaliko wa Ali Treki wa kuhudhuria mkutano mkubwa kwenye umoja wa mataifa mwezi Septemba utakaozungumzia utekelezaji wa malengo ya milennia na njia za kukabilina na umaskini ambazo viongozi duniani wameahidi kutimiza itimiapo mwaka 2015.