Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP inajiandaa kuisaidia Haiti katika uchaguzi ujao

UNDP inajiandaa kuisaidia Haiti katika uchaguzi ujao

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linajiandaa kuisaidia Haiti katika masuala ya uchaguzi baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa mapema mwaka huu.

Katika ziara yake ya tatu mwaka huu nchini Haiti tangu tetemeko la Januari 12,afisa msaidizi wa UNDP Rebeca Grynspan amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Jean-Max Bellerive na pia kuzuru miradi mbalimbali ya UNDP ya kusaidia ujenzi mpya katika mji mkuu Port-au-Prince na viunga vyake.

Bi Grynspan amesema shughuli kubwa zimefanyika baad ya kujadili na waziri mkuu mafanikio na changamoto ambazo bado zinaikabili nchi hiyo na watu wake. Ameongeza kuwa UNDP inajiandaa kuisaidia Haiti katika masuala ya kufanya uchaguzi mkuu katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya kiufundi.