Skip to main content

UNHCR yapongeza Canada ilivyoshughulikia wakimbizi waTamil

UNHCR yapongeza Canada ilivyoshughulikia wakimbizi waTamil

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaendelea kufuatilia hali ya raia 490 wa Sri Lanka kutoka kabila la Tamil, waliokuwa wasafiri wa meli ya mizigo ya MV Sun sea.

Meli hiyo ilitia nanga kwenye kisiwa cha Vancouver British Columbia nchini Canada Ijumaa iliyopita. Kama anavyofafanua Andrej Mahecici msemaji wa UNHCR watu wote wako salama na wameomba hifadhi.

(SAUTI YA MAHECIC UNHCR)

Mahecici ameongeza kuwa eneo walilopokelewa watu hao liliandaliwa vyema , walitoa maelezo yao na walipatiwa huduma muhimu kama chakula na maji. Na watu hao wote 490 ni mchanganyiko wa wanaume, wanawake na watoto.