Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha unatishia misaada Pakistan:UNICEF

Upungufu wa fedha unatishia misaada Pakistan:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema upungufu wa fedha ni kikwazo katika operesheni zake za msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan.

UNICEF inasema upungufu huo unatia hofu shughuli zake za masuala ya maji na usafi, huku mamilioni ya watoto wakiwa katika hatari ya kupata maradhi yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama. Kati ya watu zaidi ya milioni 15 walioathirika na mafuriko hayo UNICEF inasema asilimia 50 ni watoto., kama anavyofafanua Marco Rodriguez msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARCO RODRIGUEZ)

Mratibu na mwakilishi wa UNICEF nchini Pakistan Martin Mogwanja anasema kwa kuangalia idadi ya watu wanaohitaji msaada wa dharura nchini Pakistan zahma hii ni kubwa kuliko ukiunganisha kwa pamoja ilivyokuwa Tsunami, tetemeko la Haiti na lile la Pakistan.