Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeongeza msaada wa fedha kwa wanaokabiliwa na njaa Niger

UM umeongeza msaada wa fedha kwa wanaokabiliwa na njaa Niger

Katika juhudi za kumaliza tatizo la chakula lililosababisha utapia mlo wa hali ya juu miongoni mwa watoto Niger, mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetoa fedha zaidi dola milioni 15 kuinusuru Niger.

Fedha hizo ni za kulisaidia shirika la mpango wa chakula WFP kutoa msaada kwa watu takribani milioni 1.7 wanaokabiliwa na njaa. Fedha hizo zitasaidia kuboresha lishe na kuwasaidia watu walioathirika zaidi nchini humo.

Tathmini iliyofanyika mwezi April mwaka huu inaonyesha kuwa watu zaidi ya milioni 7 ambao ni sawa na asilimia 46 ya watu wote wa Niger wanakabiliwa tatizo la chakula, ikiwa ni ongezeko la watu zaidi ya milioni 3 ikilinganishwa na mwaka jana.