UNICEF kuhakikisha wanafunzi wamerejea shuleni Kyrgystan

UNICEF kuhakikisha wanafunzi wamerejea shuleni Kyrgystan

Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF na utawala wa Kyrgstan wameanzisha mpango utakaohakikisha kuwa maelfu ya wanafunzi walioathiriwa na ghasia zilizotokea katika mji wa kusini mwa nchi wa Osh wana usalama wa kurejea shuleni wakati wa kaunza kwa mwaka mpya wa masomo mwezi Septemba mwaka huu.

Mapigano ya kikabila yaliyotokea kusini mwa Kyrgyzstan mwezi Juni mwaka huu yaliathiri kwa kiasi kikubwa wanafunzi na walimu ambapo wengi walipoteza makaazi yao na kulazimika kuhama. Shirika la UNICEF linakadiria kuwa robo ya watu 400,000 walioathirika na mapigano katika miji ya Osh na Jalalabad ni watoto.

Kwa mujibu wa mashirika ya umoja wa mataifa familia nyingi kwa sasa zimerejea makwao wakati nyingi zikiwa bado zinaishi kwenye mahema. Watoto 400,000 kwa sasa wanahitaji kurejea shuleni mwezi septemba lakini nyingi ya shule zimeharibiwa.