Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetoa wito wa kurejea utulivu baada ya ghasia Ijumaa Kabul

UM umetoa wito wa kurejea utulivu baada ya ghasia Ijumaa Kabul

Umoja wa Mataifa umetoa witio wa kurejea utulivu kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul kufuatia machafuko yaliyozuka siku ya Ijumaa .

Umezitaka pande zote kusitisha ghasia na kurejesha utulivu. Duru za habari nchini humo zinasema watu wawili wameuawa katika mchafuko hayo ya kikabila yaliyozuka mjini Kabul baada ya wanakikiji wa Hazara kudaiwa kuchoma nyumba za wafugaji wa Pashtun.  Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA umetoa taarifa ukielezea hofu yake juu mvutano unaoendelea katika baadhi ya sehemu za Kabul na pia kupotea kwa maisha ya watu na uharibifu wa nyumba na mali za watu.

Taarifa ya UNAMA inasema Umoja wa Mataifa unazitaka pande zote kusitisha ghasia na kurejesha utulivu na kutekeleza sheria na amani. UNAMA ilianzishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuisaidia serikali ya Afghanistan na watu wake katika kuweka msingi wa kurejesha amani na maendeleo pia kutumia ofisi zake kuzisaidia pande zote kutatua mgogoro.