Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi unafanyika kufuatia kutekwa kwa wafanyakazi wa UNAMID

Uchunguzi unafanyika kufuatia kutekwa kwa wafanyakazi wa UNAMID

Uchunguzi unafanyika dhidi ya kutekwa kwa washauri wawili wa polisi wanaofanya kazi na vikosi vya kulinda amani Darfur vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UNAMID washauri hao walitekwa mapema jana Jumamosi kwenye eneo la Nyala ambalo ni mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini. Maafisa hao wawili ambao walitekwa wakati wakitembea kuelekea kwenye kituo cha usafiri cha UNAMID walikuwa umbali wa kilometa 100 tuu kutoka kwenye makazi yao kwenye mji wa Almatar walipozingirwa na watu watatu waliokuwa kwenye gari aina ya 4x4 .

Watekaji hao waliwachukua maafisa hao huku wakiwaonyesha bunduki na na wakaondoka nao kwa kasi kubwa. Uchunguzi dhidi ya tukio hilo unafanyika na serikali ya Sudan na UNAMID ambayo imekuwa katika eneo hilo tangu mwanzoni mwa mwaka 2008 ili kuwalinda raia na kutuliza ghasia Darfur ambapo vita vya karibu miaka saba vimekatili maisha ya watu takriban 300,000 na kuwafanya wengine milioni 2.7 kuzikimbia nyumba zao.

Tukio hili ni la karibuni kati ya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa UNAMID katika miezi ya hivi karibuni,yanayohusisha lile la mwezi jana la kushambuliwa wakiwa kwenye doria Magharibi mwa Darfur ambapo wanajeshi saba wa UNAMID walijeruhiwa, na mwezi Juni waliposhambuliwa askari watatu waliuawa na mwengine kujeruhiwa. Shambulio hili limekuja wakati ambapo kuna hofu na wasiwasi mkubwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma kufuatia duru nya karibuni ya mazungumzo ya amani yaliyofanyika mjini Doha Qatar, na baadhi ya wakimbizi wa ndani wamekuwa wakilalamika kuwa hawakuhusihswa kikamilifu