Makala kuhusu mwaka wa kimataifa wa vijana na tatizo la ajira

Makala kuhusu mwaka wa kimataifa wa vijana na tatizo la ajira

Mwaka wa kimataifa wa vijana ulizinduliwa na Umoja wa Mataifa wiki hii ambao umekwenda sambamba na siku ya kimataifa ya vijana inayoadhimishwa kila mwaka Agosti 12.

Ujumbe maalumu kutoka kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ni kuwajumuisha vijana, kuthamini mchango wao na ubunifu wao kwa maendeleo ya sasa na ya siku za usoni. Pamoja na kwamba vijana ndio idadi kubwa ya nguvu kati ya dunia kwa mujibu wa shirika la kazi duniani ILO wengi hawana ajira. Vijana milioni 620 wanaostahili kuwa kazini hadi mwishoni mwa mwaka jana milioni 87 hawakuwa na ajira, suala linalotia hofu kubwa hasa kwa maendeleo.

Tatizo hilo linayakabili mabara yote lakini Afrika inaonekana kuwa msitari wa mbele. Nchini Burundi mwandishi wetu Ramadhani Kibuga amepita mitaani kuzungumza na vijana mbalimbali kuhusu tatizo hilo la ajira ambako amebaini kuwa siku hizi ni jambo la kawaida katika mitaa ya Bujumbura kuwakuta vijana wakizurura na stashahada na shahada zao za vyuo vikuu bila kazi. Ungana naye katika makala hii.