Kamati ya UM ya uchunguzi wa flotilla imeeleza mipango yake

Kamati ya UM ya uchunguzi wa flotilla imeeleza mipango yake

Kamati ya uchunguzi iliyoteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki moon kufanya uchunguzi kuhusiana na uvamizi kwenye msafara wa meli uliokuwa ukielekea katika ukanda wa Gaza na wanajeshi wa Israel, itakutana tena mapema mwezi ujao baada ya kuanza mazungumzo juma hili kujadili jinsi itakavyoendesha uchunguzi huo.

Kamati hiyo ya wanachama wanne ilikutano na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bak ki moon na idara zingine za umoja huo juma hili mjini New York kwa muda wa siku mbili .

Kamati hiyo ina jukumu la kubaini ukweli kuhusu kile ambacho kilijiri wakati wa uvamizi kwenye msafara huo wa meli uliokuwa safariki kutoka Uturuki kwenda ukanda wa Gaza. Kamati hiyo inaongozwa na waziri mkuu wa zamani wa new Zealand Geoffrey Palmer akisaidiwa na aliyekuwa rais wa Colombia Alvaro Uribe wakiwemo pia waakilishi wawili kutoka Israel na uturuki.