Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq yahitaji kupiga hatua kubwa kimaendeleo wasema UM

Iraq yahitaji kupiga hatua kubwa kimaendeleo wasema UM

Ripoti mpya ya umoja wa mataifa na Iraq inaonyesha kuwa Iraq inahitaji kupiga hatua katika masuala ya kimaendeleo.

Masuala hayo ni pamoja na kukabiliana na njaa, kupunguza vifo vya watoto na pia katika juhudi za kujiunga kwa wanafanzi zaidi katika shule za msingi na pia kuwepo kwa maji na mazingira safi. Pande hizo pia zimekubaliana kufanya mikakati ya kutimiza masuala kadha itimiapo mwaka 2015 ambao ni mwaka wa kuafikiwa kwa malengo wa milenia yakiwemo ya kumaliza umasikini, kupunga vifo vya watoto pamoja na magonjwa.

Mratibu wa huduma za kibinadamau wa umoja wa mataifa nchini Iraq Christine mcNab amesema kwamba malengo ya milenia nchini Iraq yanahusu maisha mema ya baadaye ya wananchi wa Iraq. Amesema kuisadia Iraq kutimiza malengo yake ya milenia ni moja ya ajenda kuu ya umoja wa matifa suala ambalo litawahakikishia maisha mema mamilioni ya Wairaq hasa vijana na watoto.