Hofu yawakumba wakulima Madagascar baada ya kuzuka nzige:UM
Shirika la chakula na kilimo FAO leo limeonya kuwa Madascar iko katika hatari ya mlipuko wa nzige na kutishia maisha ya watu 460, 000 walioko vijijini.
Shirika hilo linasema idadi isiyojulikana na nzige katika eneo la Malagasy wamehama kutoka upande wa Kusini magharibi ambako mara nyingi hudhibitiwa na kusambaa katika maeneo ya mashariki na Kaskazini.
FAO leo imesema kwamba kampeni kubwa ya angani na ardhini ambayo ni ya muda mrefu inahitajika kabla ya msimu wa mvua kuanza Madgascar ambao kwa kawaida huwa ni kuanzia katikati ya Oktoba, ili kuinusuru nchi hiyo na athari kubwa za nzige.