Skip to main content

UM wataka taarifa kutoka kwa Hizbollah kuhusu mauaji ya Hariri

UM wataka taarifa kutoka kwa Hizbollah kuhusu mauaji ya Hariri

Mwendesha mashitaka katika mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa , iliyoundwa ili kuwahukumu washukiwa wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri na wengine 22 imwitaka serikali kukabidhi taarifa zote zinazodaiwa kuhifadhiwa na kiongozi wa Hisbollah Hassan Nasrallah ambazo ni muhimu kwa ajili ya tukio hilo la 2005.

Baadhi ya vitu vinavyotakiwa kuabidhiwa ni pamoja na video iliyoonyeshwa kwenye televisheni wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na nyaraka zingine zozote ambazo zitasaidia ofisi ya waendesha mashitaka kubaini ukweli. Ofisi hiyo pia imemualika bwana Nasrallah kutumia mamlaka yake kusaidia katika uchunguzi.

Mahakama hiyo ni chombo huru na ilianzishwa The Haugue kufuatia uchunguzi wa tume huru ya kimataifa baada ya uchunguzi wa awali wa mpango wa Umoja wa Mataifa kubaini kwamba uchunguzi wa Lebanon kuhusu shambulio hilo la Februari 2005 ulikuwa na dosari nyingi na kwamba Syria ilionekana kuwa chanzo cha mvutano wa kisiasa uliopolekea shambulio hilo.