Mcheza filamu wa Bollywood awa Balozi Mwema wa haki za watoto na vijana
Mmoja wa wacheza filamu mashuhuri wa India Priyanka Chopra ameteuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuwa balozi wake mwema mpya kwa jukumu la kuchagiza masuala ya haki za watoto na vijana wadogo.
Bi Chopra ambaye aliwahi kuwa mshindi wa taji la urembo la dunia aliingia katika uwanja wa filamu mwaka 2002 na tangu hapo amekuwa akitumia kipaji chake mbali ya kuburudisha jamii lakini pia kuilelimisha.