UNEP inatathimini mafuta yanayovuja kwenye jimbo la Niger Delta Nigeria

UNEP inatathimini mafuta yanayovuja kwenye jimbo la Niger Delta Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP linaendelea na mipango yake ya kina ya mazingira kwa kutathimini chanzo cha athari za kuviua kwa mafuta katika jimbo la Niger Delta nchini Nigeria.

Mike Cowing afisa wa UNEP akitoa taarifa kuhusu tathimini ya kuvuja kwa mafuta katika eneo la Ogoniland jimbo la Niger Delta amesema mwaka 2007 serikali ya Nigeria iliiomba UNEP kufanya utafiti katika jimbo hilo kwa sababu waliona kwamba kushughulikia matatizo ya mazingira yanayosababishwa na kuvuja kwa mafuta na athari zake kwa afya ya jamii kutasaidia amani katika eneo hilo.

Mike amesema UNEP na timu yake ya watu zaidi ya 100 walianza utafiti huo Oktoba mwaka jana ili kuona athari zake katika eneo la Ogoniland. Amesema wanachukua udongo, maji, mafuta na vipimo vya binadamu ili kupeleka maabara kufifanyia uchunguzi ili kupata ukweli wa athari za mafuta hayo kwa binadamu na mazingira Niger Delta.