Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imezindua mfumo wa NASA ili kubaini vyanzo vya moto

FAO imezindua mfumo wa NASA ili kubaini vyanzo vya moto

Shirika la chakula na kilimo FAO limezindua mfumo wa NASA wa kuzisaidia nchi kubaini vyanzo vya moto katika wakati unaofaa.

Mfumo huo uliozinduliwa leo ni wa njia ya kutumia wavuti na unatoa taarifa muhimu kuhusu moto na utazisaidia nchi kudhibiti moto vyema na kulinda majengo na mali asili. Mfumo huo waliouita ‘mfumo wa kimataifa wa taarifa za moto' GFIMS, utaweza kubaini vyanzo vya moto kwa njia ya satellite kwa kutumia mfumo wa Marekani wa NASA.

Mfumo huo ambao umeanzishwa kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Maryland una ramani kwenye wavuti ambayo inaonyesha maeneo ambayo ni vyanzo vya moto na utawasaidia watumiaji kupokea barua pepe ya kuwaonya kuhusu maeneo fulani na itasaidia kuchukua hatua haraka.

Kwa mujibu wa FAO moto wa msituni huteketeza takribani ekari milioni 350 duniani kote kila mwaka na hivyo ni muafaka kwa watu na mazingira kulindwa kwani ni muhimu kuthibiti moto huo.